19. BWANA ameweka kiti chake cha enzi mbinguni,Na ufalme wake unavitawala vitu vyote.
20. Mhimidini BWANA, enyi malaika zake,Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake,Mkiisikiliza sauti ya neno lake.
21. Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote,Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake.