15. Mwanadamu siku zake zi kama majani;Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo.
16. Maana upepo hupita juu yake, kumbe haliko!Na mahali pake hapatalijua tena.
17. Bali fadhili za BWANA zina wamchaoTangu milele hata milele,Na haki yake ina wana wa wana;
18. Maana, wale walishikao agano lake,Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye.
19. BWANA ameweka kiti chake cha enzi mbinguni,Na ufalme wake unavitawala vitu vyote.
20. Mhimidini BWANA, enyi malaika zake,Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake,Mkiisikiliza sauti ya neno lake.
21. Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote,Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake.