Zab. 102:18-27 Swahili Union Version (SUV)

18. Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo,Na watu watakaoumbwa watamsifu BWANA.

19. Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu,Toka mbinguni BWANA ameiangalia nchi,

20. Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa,Na kuwafungua walioandikiwa kufa.

21. Watu walitangaze jina la BWANA katika Sayuni,Na sifa zake katika Yerusalemu,

22. Pindi mataifa watapokusanyika pamoja,Falme nazo ili kumtumikia BWANA.

23. Amezipunguza nguvu zangu njiani;Amezifupisha siku zangu.

24. Nitasema, Ee Mungu wangu, usiniondoe katikati ya siku zangu;Miaka yako ni tangu kizazi hata kizazi.

25. Hapo mwanzo uliutia msingi wa nchi,Na mbingu ni kazi ya mikono yako.

26. Hizi zitaharibika, bali Wewe utadumuNaam, hizi zitachakaa kama nguo;Na kama mavazi utazibadilisha,Nazo zitabadilika.

27. Lakini Wewe U Yeye yule;Na miaka yako haitakoma.

Zab. 102