1. Ndipo Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki,
2. Akasema,Nalimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu,Naye akaniitikia;Katika tumbo la kuzimu naliomba,Nawe ukasikia sauti yangu.
3. Maana ulinitupa vilindini,Ndani ya moyo wa bahari;Gharika ya maji ikanizunguka pande zote;Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.
4. Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako;Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.
5. Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu;Vilindi vilinizunguka;Mwani ulikizinga kichwa changu;
6. Nalishuka hata pande za chini za milima;Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele;Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni,Ee BWANA, Mungu wangu,
7. Roho yangu ilipozimia ndani yangu,Nalimkumbuka BWANA;Maombi yangu yakakuwasilia,Katika hekalu lako takatifu.