15. Ole wake siku hii!Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi.
16. Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu?
17. Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; ghala zimeachwa ukiwa; mabanda yamevunjika; kwa maana nafaka imekauka.
18. Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng’ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya kondoo yamepata mateso.
19. Ee BWANA, nakulilia wewe;Kwa maana moto umeyala malisho ya nyikani,Na miali ya moto imeteketeza miti yote ya mashamba.
20. Naam, wanyama wa mashamba wanakutwetea wewe;Kwa maana vijito vya maji vimekauka,Na moto umeyateketeza malisho ya nyikani.