1. Neno hili ndilo alilosema BWANA, katika habari za Babeli, na katika habari za Wakaldayo, kwa kinywa cha Yeremia, nabii.
2. Tangazeni katika mataifa,Mkahubiri na kutweka bendera;Hubirini, msifiche, semeni,Babeli umetwaliwa!Beli amefedheheka;Merodaki amefadhaika;Sanamu zake zimeaibishwa,Vinyago vyake vimefadhaika.
3. Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hapana mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia.
4. Katika siku hizo, na wakati huo, asema BWANA, wana wa Israeli watakuja, wao na wana wa Yuda pamoja; Wataendelea njiani mwao wakilia, nao watamtafuta BWANA, Mungu wao.
5. Watauliza habari za Sayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njoni ninyi, mjiunge na BWANA, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa.
6. Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika.
7. Watu wote waliowaona wamewala; na adui zao walisema, Sisi hatuna hatia, kwa kuwa hao wametenda dhambi juu ya BWANA, aliye kao la haki, yaani, BWANA, tumaini la baba zao.
8. Kimbieni kutoka kati ya Babeli, mkatoke katika nchi ya Wakaldayo, mkawe kama mabeberu mbele ya makundi.
9. Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hapana hata mmoja utakaorudi bure.