21. Na watu wake waliojiwa, walio kati yake,Ni kama ndama waliowanda malishoni;Maana wao nao wamerudi nyuma,Wamekimbia wote pamoja, wasisimame;Maana siku ya msiba wao imewafikilia,Wakati wa kujiliwa kwao.
22. Sauti yake ni kama nyoka, wajapo kwa nguvu,Watamjia na mashoka, kama wachanja kuni.
23. Wataukata msitu wake, asema BWANA, ingawa haupenyeki;Kwa maana ni wengi kuliko nzige, hawahesabiki.
24. Binti ya Misri ataaibishwa;Atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.
25. BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Amoni wa No, na Farao, na Misri, pamoja na miungu yake, na wafalme wake, naam, Farao, na hao wanaomtumainia;
26. nami nitawatia katika mikono ya hao wanaowatafuta roho zao, na katika mikono ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya watumishi wake; na baada ya hayo itakaliwa na watu, kama katika siku za kale, asema BWANA.