18. Basi, BWANA asema hivi, katika habari ya Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake.
19. Atazikwa maziko ya punda, akibururwa, na kutupwa nje ya malango ya Yerusalemu.
20. Haya panda Lebanoni, ukalieUpalize sauti yako katika Bashani;Ukalie kutoka Abarimu;Maana wapenzi wako wote wameangamia.
21. Mimi nalisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutokuitii sauti yangu.
22. Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na wapenzi wako watakwenda kufungwa; hakika wakati huo utatahayarika, na kufadhaika kwa sababu ya uovu wako wote.
23. Wewe ukaaye Lebanoni,Ufanyaye kioto chako katika mierezi,Utakuwa na hali ya kuhurumiwa sana,Upatapo utungu kama wa mwanamke azaaye.
24. Kama niishivyo mimi, asema BWANA, hata Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, angekuwa pete yenye muhuri katika mkono wangu wa kuume, ningekung’oa wewe hapo;
25. nami nitakutia katika mikono ya watu wale wakutafutao roho yako, na katika mikono yao unaowaogopa, naam, katika mikono ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya Wakaldayo.
26. Nami nitakutupa nje, wewe na mama yako aliyekuzaa, mwende nchi nyingine ambayo hamkuzaliwa huko, nanyi mtakufa huko.
27. Lakini nchi ile ambayo wanatamani kuirudia, hawatairudia kamwe.
28. Je! Mtu huyu, Konia, ni chombo kilichodharauliwa, na kuvunjika? Ni chombo kisichopendeza? Mbona wametupwa, yeye na wazao wake, na kutupwa katika nchi wasiyoijua?
29. Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la BWANA.
30. BWANA asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.