Wim. 6:8-12 Swahili Union Version (SUV)

8. Wako malkia sitini, na masuria themanini,Na wanawali wasiohesabika;

9. Hua wangu, mkamilifu wangu, ni mmoja tu,Mtoto wa pekee wa mamaye.Ndiye kipenzi chake aliyemzaa,Binti wakamwona wakamwita heri;Malkia na masuria nao wakamwona,Wakamsifu, wakisema,

10. Ni nani huyu atazamaye kama alfajiri,Mzuri kama mwezi, safi kama jua,Wa kutisha kama wenye bendera?

11. Nalishukia bustani ya milozi,Ili kuyatazama machipuko ya bondeni;Nione kama mzabibu umechanua,Kama mikomamanga imetoa maua.

12. Kabla sijajua, roho yangu iliniletaKatikati ya magari ya wakuu wangu.

Wim. 6