5. Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera,Kwa maana nimezimia kwa mapenzi.
6. Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,Nao wa kuume unanikumbatia!
7. Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Kwa paa na kwa ayala wa porini,Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,Hata yatakapoona vema yenyewe.
8. Sikiliza! Ni mpendwa wangu! Tazama, anakuja,Akiruka milimani, akichachawa vilimani.
9. Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala.Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu,Achungulia dirishani, atazama kimiani.
10. Mpendwa wangu alinena, akaniambia,Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako,
11. Maana tazama, kaskazi imepita,Masika imekwisha, imekwenda zake;
12. Maua yatokea katika nchi,Wakati wa kupelea umefika,Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu.
13. Mtini wapevusha tini zake,Na mizabibu inachanua,Inatoa harufu yake nzuri;Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.
14. Hua wangu, mafichoni mwa jabali,Katika sitara za magenge,Nitazame uso wako, nisikie sauti yako,Maana sauti yako ni tamu na uso wako mzuri.