Sef. 3:14-20 Swahili Union Version (SUV)

14. Imba, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee Israeli;Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, Ee binti Yerusalemu.

15. BWANA ameziondoa hukumu zako,Amemtupa nje adui yako;Mfalme wa Israeli, naam, yeye BWANA, yu katikati yako;Hutaogopa uovu tena.

16. Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa,Usiogope, Ee Sayuni; mikono yako isilegee.

17. BWANA, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa;Atakushangilia kwa furaha kuu,Atakutuliza katika upendo wake,Atakufurahia kwa kuimba.

18. Nitawakusanya wanaousikitikia mkutano wa ibada, hao waliokuwa wa kwako; ambao mzigo uliokuwa juu yake ulikuwa fedheha kwao.

19. Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya kuwa sifa na jina, hao ambao fedheha yao ilikuwa katika dunia yote.

20. Wakati huo nitawaingizeni, na wakati huo nitawakusanya; kwa maana nitawafanya ninyi kuwa sifa na jina, miongoni mwa watu wote wa dunia, nitakapowarudisha wafungwa wenu mbele ya macho yenu, asema BWANA.

Sef. 3