Huu ndio mji ule wa furaha,Uliokaa pasipo kufikiri,Uliosema moyoni mwake, Mimi niko,Wala hapana mwingine ila mimi.Jinsi ulivyokuwa ukiwa,Mahali pa kulala pa wanyama wa bara!Kila mtu apitaye atazomea,Na kutikisa mkono wake.