Omb. 4:5-11 Swahili Union Version (SUV)

5. Wale waliokula vitu vya anasaWameachwa peke yao njiani;Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekunduWakumbatia jaa.

6. Maana uovu wa binti ya watu wangu ni mkubwaKuliko dhambi ya Sodoma,Uliopinduliwa kama katika dakika moja,Wala mikono haikuwekwa juu yake.

7. Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji,Walikuwa weupe kuliko maziwa;Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani,Na umbo lao kama yakuti samawi.

8. Nyuso zao ni nyeusi kuliko makaa;Hawajulikani katika njia kuu;Ngozi yao yagandamana na mifupa yaoImekauka, imekuwa kama mti.

9. Heri wale waliouawa kwa upangaKuliko wao waliouawa kwa njaa;Maana hao husinyaa, wakichomwaKwa kukosa matunda ya mashamba.

10. Mikono ya wanawake wenye hurumaImewatokosa watoto wao wenyewe;Walikuwa ndio chakula chaoKatika uharibifu wa binti ya watu wangu.

11. BWANA ameitimiza kani yake,Ameimimina hasira yake kali;Naye amewasha moto katika SayuniUlioiteketeza misingi yake.

Omb. 4