Omb. 2:5-9 Swahili Union Version (SUV)

5. Bwana amekuwa mfano wa adui,Amemmeza Israeli;Ameyameza majumba yake yote,Ameziharibu ngome zake;Tena amemzidishia binti YudaMatanga na maombolezo.

6. Naye ameondoa maskani yake kwa nguvu,Kana kwamba ni ya bustani tu;Ameziharibu sikukuu zake;BWANA amezisahauzisha katika SayuniSikukuu za makini na sabato;Naye amewadharau mfalme na kuhaniKatika uchungu wa hasira yake.

7. Bwana ameitupilia mbali madhabahu yake,Amepachukia patakatifu pake;Amezitia katika mikono ya hao aduiKuta za majumba yake;Wamepiga kelele ndani ya nyumba ya BWANAKama katika siku ya kusanyiko la makini.

8. BWANA amekusudia kuuharibuUkuta wa binti Sayuni;Ameinyosha hiyo kamba,Hakuuzuia mkono wake usiangamize;Bali amefanya boma na ukuta kuomboleza;Zote pamoja hudhoofika.

9. Malango yake yamezama katika nchi;Ameyaharibu makomeo yake na kuyavunja;Mfalme wake na wakuu wake wanakaaKati ya mataifa wasio na sheria;Naam, manabii wake hawapati maonoYatokayo kwa BWANA.

Omb. 2