15. Hao watu wote wapitaoHukupigia makofi;Humzomea binti Yerusalemu,Na kutikisa vichwa vyao;Je! Mji huu ndio ulioitwa, Ukamilifu wa uzuri,Furaha ya dunia yote?
16. Juu yako adui zako woteWamepanua vinywa vyao;Huzomea, husaga meno yao,Husema, Tumemmeza;Hakika siku hii ndiyo tuliyoitazamia;Tumeipata, tumeiona.
17. BWANA ameyatenda aliyoyakusudia; amelitimiza neno lake,Aliloliamuru siku za kale;Ameangusha hata chini,Wala hakuona huruma;Naye amemfurahisha adui juu yako,Ameitukuza pembe ya watesi wako.
18. Mioyo yao ilimlilia Bwana;Ee ukuta wa binti Sayuni!Machozi na yachuruzike kama mtoMchana na usiku;Usijipatie kupumzika;Mboni ya jicho lako isikome.
19. Inuka, ulalamike usiku,Mwanzo wa makesha yake;Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana;Umwinulie mikono yako;Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa,Mwanzo wa kila njia kuu.
20. Tazama, BWANA, uangalie,Ni nani uliyemtenda hayo!Je! Wanawake wale mazao yao,Watoto waliowabeba?Je! Kuhani na nabii wauaweKatika patakatifu pa Bwana?
21. Kijana na mzee hulala chiniKatika njia kuu;Wasichana wangu na wavulana wanguWameanguka kwa upanga;Umewaua katika siku ya hasira yako;Umeua, wala hukuona huruma.
22. Umeziita kama katika siku ya mkutano wa makini;Hofu zangu zije pande zote;Wala hapana hata mmoja aliyepona wala kusaliaKatika siku ya hasira ya BWANA;Hao niliowabeba na kuwaleaHuyo adui yangu amewakomesha.