Mt. 26:64-74 Swahili Union Version (SUV)

64. Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.

65. Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake;

66. mwaonaje ninyi? Wakajibu, wakasema, Imempasa kuuawa.

67. Ndipo wakamtemea mate ya uso, wakampiga makonde; wengine wakampiga makofi,

68. wakisema, Ewe Kristo, tufumbulie; ni nani aliyekupiga?

69. Na Petro alikuwa ameketi nje behewani; kijakazi mmoja akamwendea, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya.

70. Akakana mbele ya wote, akisema, Sijui usemalo.

71. Naye alipotoka nje hata ukumbini, mwanamke mwingine alimwona, akawaambia watu waliokuwako huko, Huyu alikuwapo pamoja na Yesu Mnazareti.

72. Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu.

73. Punde kidogo, wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha.

74. Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema, Simjui mtu huyu. Na mara akawika jogoo.

Mt. 26