17. Kwa kuwa mtego hutegwa bure,Mbele ya macho ya ndege ye yote.
18. Na hao hujiotea damu yao wenyewe,Hujinyemelea nafsi zao wenyewe.
19. Ndivyo zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali;Huuondoa uhai wao walio nayo.
20. Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu,Hutoa sauti yake katika viwanja;
21. Hulia penye mikutano mikubwa ya watu,Mahali pa kuyaingilia malango,Ndani ya mji hutamka maneno yake.
22. Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga?Na wenye dharau kupenda dharau yao,Na wapumbavu kuchukia maarifa?
23. Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu;Tazama, nitawamwagia roho yangu,Na kuwajulisheni maneno yangu.
24. Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa;Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu;