1. Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi;Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.
2. Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume;Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto.
3. Naam, huyo mpumbavu tena, aendapo njiani, hupungukiwa na fahamu zake; hata humwambia kila mtu ya kuwa yeye ni mpumbavu.
4. Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako,Usiondoke mara mahali pako ulipo;Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.
5. Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye;
6. ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini.
7. Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.