8. Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi;
9. wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani.
10. Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua.
11. Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.
12. Basi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa.
13. Na hao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akisema, Ndugu zangu, nisikilizeni.
14. Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake.
15. Na maneno ya manabii yapatana na hayo, kama ilivyoandikwa,
16. Baada ya mambo haya nitarejea,Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka.Nitajenga tena maanguko yake,Nami nitaisimamisha;
17. Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana,Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao;
18. Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele.
19. Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa;
20. bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu.
21. Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.
22. Basi ikawapendeza mitume na wazee na kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba; nao ni hawa, Yuda aliyeitwa Barsaba, na Sila, waliokuwa watu wakuu katika ndugu. Wakaandika hivi na kupeleka kwa mikono yao,