6. Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo.
7. Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini.
8. Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi;
9. wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani.
10. Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua.
11. Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.
12. Basi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa.
13. Na hao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akisema, Ndugu zangu, nisikilizeni.
14. Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake.
15. Na maneno ya manabii yapatana na hayo, kama ilivyoandikwa,
16. Baada ya mambo haya nitarejea,Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka.Nitajenga tena maanguko yake,Nami nitaisimamisha;
17. Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana,Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao;
18. Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele.