32. Na sisi tunawahubiri habari njema ya ahadi ile waliyopewa mababa,
33. ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu; kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili,Wewe ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa.
34. Tena ya kuwa alimfufua katika wafu, asipate kurudia uharibifu, amenena hivi,Nitawapa ninyi mambo matakatifu ya Daudi yaliyo amini.
35. Kwa hiyo anena na pengine,Hutamwachia Mtakatifu wako kuona uharibifu.
36. Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.
37. Bali huyu aliyefufuliwa na Mungu hakuona uharibifu.
38. Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi;
39. na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.
40. Angalieni, basi, isiwajilie habari ile iliyonenwa katika manabii.
41. Tazameni, enyi mnaodharau, kastaajabuni, mkatoweke; kwa kuwa natenda kazi mimi siku zenu, kazi ambayo msingeisadiki kabisa, ijapo mtu akiwasimulia sana.
42. Na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya sabato ya pili.
43. Sinagogi ilipofumukana, Wayahudi na waongofu watauwa wengi wakashikamana na Paulo na Barnaba; ambao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu.
44. Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.