Lk. 10:26-36 Swahili Union Version (SUV)

26. Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?

27. Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

28. Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.

29. Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani?

30. Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa.

31. Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.

32. Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.

33. Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,

34. akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.

35. Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.

36. Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi?

Lk. 10