1. Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake.
2. Akasema,BWANA alitoka Sinai,Akawaondokea kutoka Seiri;Aliangaza katika kilima cha Parani,Akaja Meribath-kadeshi.Upande wa mkono wake wa kuumePalikuwa na sheria ya moto-moto kwao.
3. Hakika awapenda hayo makabila ya watu;Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako;Nao waliketi miguuni pako;Watapokea kila mmoja katika maneno yako.