1. Lakini yeye aliyekuwa katika dhiki hatakosa changamko. Hapo kwanza aliiingiza nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali katika hali ya kudharauliwa, lakini zamani za mwisho ameifanya kuwa tukufu, karibu na njia ya bahari; ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa.
2. Watu wale waliokwenda katika gizaWameona nuru kuu;Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti,Nuru imewaangaza.
3. Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao;Wanafurahi mbele zako,Kama furaha ya wakati wa mavuno,Kama watu wafurahivyo wagawanyapo nyara.
4. Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake, na gongo la bega lake, na fimbo yake yeye aliyemwonea, kama katika siku ya Midiani.