Isa. 62:8-12 Swahili Union Version (SUV)

8. BWANA ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi.

9. Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.

10. Piteni, piteni, katika malango;Itengenezeni njia ya watu;Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake;Twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu.

11. Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia,Mwambieni binti Sayuni,Tazama, wokovu wako unakuja;Tazama, thawabu yake i pamoja naye,Na malipo yake yako mbele zake.

12. Nao watawaita, Watu watakatifu,Waliokombolewa na BWANA;Nawe utaitwa, Aliyetafutwa,Mji usioachwa.

Isa. 62