Isa. 62:7-12 Swahili Union Version (SUV)

7. wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani.

8. BWANA ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi.

9. Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.

10. Piteni, piteni, katika malango;Itengenezeni njia ya watu;Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake;Twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu.

11. Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia,Mwambieni binti Sayuni,Tazama, wokovu wako unakuja;Tazama, thawabu yake i pamoja naye,Na malipo yake yako mbele zake.

12. Nao watawaita, Watu watakatifu,Waliokombolewa na BWANA;Nawe utaitwa, Aliyetafutwa,Mji usioachwa.

Isa. 62