Isa. 55:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Haya, kila aonaye kiu, njoni majini,Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle;Naam, njoni, nunueni divai na maziwa,Bila fedha na bila thamani.

2. Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula?Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha?Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema,Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.

3. Tegeni masikio yenu, na kunijia;Sikieni, na nafsi zenu zitaishi;Nami nitafanya nanyi agano la milele,Naam, rehema za Daudi zilizo imara.

4. Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa kabila za watu.

5. Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.

6. Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana,Mwiteni, maadamu yu karibu;

7. Mtu mbaya na aache njia yake,Na mtu asiye haki aache mawazo yake;Na amrudie BWANA,Naye atamrehemu;Na arejee kwa Mungu wetu,Naye atamsamehe kabisa.

8. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.

Isa. 55