1. Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu.
2. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.
3. Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye,Itengenezeni nyikani njia ya BWANA;Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
4. Kila bonde litainuliwa,Na kila mlima na kilima kitashushwa;Palipopotoka patakuwa pamenyoka,Na palipoparuza patasawazishwa;
5. Na utukufu wa BWANA utafunuliwa,Na wote wenye mwili watauona pamoja;Kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.
6. Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia!Nikasema,Nilie nini? Wote wenye mwili ni majani,Na wema wake wote ni kama ua la kondeni;
7. Majani yakauka, ua lanyauka;Kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake.Yakini watu hawa ni majani.
8. Majani yakauka, ua lanyauka;Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.
9. Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema,Panda juu ya mlima mrefu;Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema,Paza sauti kwa nguvu;Paza sauti yako, usiogope;Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu.
10. Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa,Na mkono wake ndio utakaomtawalia;Tazameni, thawabu yake i pamoja naye,Na ijara yake i mbele zake.
11. Atalilisha kundi lake kama mchungaji,Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake;Na kuwachukua kifuani mwake,Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.