8. Tazama, nitakirudisha nyuma kivuli madaraja kumi, ambayo kilishuka juu ya duara ya Ahazi kwa sababu ya jua. Basi jua likarudi madaraja kumi katika hiyo duara, ambayo limekwisha kushuka.
9. Haya ndiyo maandiko ya Hezekia, mfalme wa Yuda, alipokuwa hawezi, naye akapona ugonjwa wake.
10. Nalisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu;Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.
11. Nalisema, Sitamwona BWANA, yeye BWANA, katika nchi ya walio hai;Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.
12. Kao langu limeondolewa kabisa,limechukuliwa kama hema ya mchungaji;Nimekunja maisha yangu kama mfumaji;atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi;Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
13. Nalijituliza hata asubuhi;kama simba, aivunja mifupa yangu yote;Tangu mchana hata usiku wanimaliza.