13. Juu ya nchi ya watu wangu itamea michongoma na mibigili; naam, juu ya nyumba za furaha katika mji ulio na shangwe;
14. maana jumba la mfalme litaachwa; mji uliokuwa na watu wengi utakuwa hauna mtu; kilima na mnara utakuwa makao ya wanyama milele, furaha ya punda-mwitu, malisho ya makundi ya kondoo;
15. hata roho itakapomwagwa juu yetu kutoka juu; hata jangwa litakapokuwa shamba lizaalo sana; nalo shamba lizaalo sana litakapohesabiwa kuwa msitu.
16. Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki itakaa katika shamba lizaalo sana.
17. Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.
18. Na watu wangu watakaa katika kao la amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu.
19. Lakini mvua ya mawe itakunya, wakati wa kuangushwa miti ya msituni; na huo mji utadhilika.
20. Heri ninyi mpandao mbegu kando ya maji yote, na kuiacha miguu ya ng’ombe na punda waende ko kote.