Hes. 21:27-35 Swahili Union Version (SUV)

27. Kwa hiyo, hao wanenao kwa mithali wasema,Njoni Heshboni,Mji wa Sihoni na ujengwe na kuthibitishwa;

28. Maana, moto umetoka Heshboni,Umekuwa Ari ya Moabu,Mwali wa moto umetoka mji wa Sihoni;Wakuu wa mahali palipoinuka Arnoni

29. Ole wako Moabu!Umeangamia, enyi watu wa Kemoshi;Amewatoa wanawe kuwa wakimbizi,Na binti zake waende utumwani,Wamwendee Sihoni mfalme wa Waamori.

30. Tumewapigia mishale; Heshboni umepotea mpaka Diboni,Nasi tumeharibu mpaka Nofa,Ifikiliayo Medeba.

31. Basi hivyo Israeli akaketi katika nchi ya Waamori.

32. Kisha Musa akapeleka watu ili kupeleleza Yazeri, nao wakaitwaa miji yake, wakawafukuza Waamori waliokuwamo.

33. Kisha wakageuka na kukwea kwa njia ya Bashani; na Ogu mfalme wa Bashani akaondoka apigane nao huko Edrei, yeye na watu wake wote.

34. BWANA akamwambia Musa, Usimche; kwa kuwa nimekwisha mtia mkononi mwako, na watu wake wote, na nchi yake; nawe utamtenda kama ulivyomtenda Sihoni mfalme wa Waamori, aliyeketi Heshboni.

35. Basi wakampiga, na wanawe, na watu wake wote, hata wasisaze kwake mtu ye yote; nao wakaimiliki nchi yake.

Hes. 21