Hes. 21:25-33 Swahili Union Version (SUV)

25. Basi Israeli wakaitwaa miji hiyo yote; Israeli wakakaa katika miji yote ya Waamori, katika Heshboni, na miji yake yote.

26. Kwa kuwa Heshboni ulikuwa ni mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akipigana na mfalme wa Moabu wa mbele, na kumpokonya nchi yake yote mkononi mwake, mpaka mto wa Arnoni.

27. Kwa hiyo, hao wanenao kwa mithali wasema,Njoni Heshboni,Mji wa Sihoni na ujengwe na kuthibitishwa;

28. Maana, moto umetoka Heshboni,Umekuwa Ari ya Moabu,Mwali wa moto umetoka mji wa Sihoni;Wakuu wa mahali palipoinuka Arnoni

29. Ole wako Moabu!Umeangamia, enyi watu wa Kemoshi;Amewatoa wanawe kuwa wakimbizi,Na binti zake waende utumwani,Wamwendee Sihoni mfalme wa Waamori.

30. Tumewapigia mishale; Heshboni umepotea mpaka Diboni,Nasi tumeharibu mpaka Nofa,Ifikiliayo Medeba.

31. Basi hivyo Israeli akaketi katika nchi ya Waamori.

32. Kisha Musa akapeleka watu ili kupeleleza Yazeri, nao wakaitwaa miji yake, wakawafukuza Waamori waliokuwamo.

33. Kisha wakageuka na kukwea kwa njia ya Bashani; na Ogu mfalme wa Bashani akaondoka apigane nao huko Edrei, yeye na watu wake wote.

Hes. 21