5. watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.
6. Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.
7. Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.
8. Maana, awalaumupo, asemaAngalia, siku zinakuja, asema Bwana,Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya;
9. Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao,Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri.Kwa sababu hawakudumu katika agano langu,Mimi nami sikuwajali asema Bwana.
10. Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya IsraeliBaada ya siku zile, asema Bwana;Nitawapa sheria zangu katika nia zao,Na katika mioyo yao nitaziandika;Nami nitakuwa Mungu kwao,Nao watakuwa watu wangu.
11. Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake,Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana;Kwa maana wote watanijua,Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.
12. Kwa sababu nitawasamehe maovu yao,Na dhambi zao sitazikumbuka tena.