4. BWANA, ulipotoka katika Seiri,Ulipokwenda vitani kutoka mashamba ya Edomu,Nchi ilitetema, mbingu nazo zikadondoza maji,Naam, mawingu yakadondoza maji.
5. Milima ikayeyuka mbele za uso wa BWANA,Naam hata Sinai ule mbele za uso wa BWANA, Mungu wa Israeli.
6. Katika siku za Shamgari, mwana wa Anathi,Siku za Yaeli, njia kuu zilikuwa hazina watu;Nao wenye kusafiri walipita kwa njia za kando.
7. Maliwali walikoma katika Israeli, walikoma,Hata mimi Debora nilipoinuka,Nilipoinuka mimi, mama katika Israeli.
8. Walichagua miungu mipya,Ndipo kulikuwa na vita malangoni;Je! Ilionekana ngao au mkukiKatika watu elfu arobaini wa Israeli?
9. Moyo wangu unawaelekea maliwali wa Israeli,Waliojitoa nafsi zao kwa hiari yao miongoni mwa watu;Mhimidini BWANA.
10. Itangazeni habari, ninyi mpandao punda weupe,Ninyi mketio juu ya mazulia ya thamani,Na ninyi mnaopita njiani kwa miguu.