20. Walipigana kutoka mbinguni,Nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera.
21. Mto ule wa Kishoni uliwachukua,Ule mto wa zamani, mto wa Kishoni.Ee roho yangu, endelea mbele kwa nguvu.
22. Ndipo kwato za farasi zilikanyaga-kanyagaKwa sababu ya kupara-para,Kupara-para kwao wenye nguvu.
23. Ulaanini Merozi, alisema malaika wa BWANA,Walaanini kwa uchungu wenyeji wake;Kwa maana hawakuja kumsaidia BWANA,Kumsaidia BWANA juu ya hao wenye nguvu.
24. Atabarikiwa Yaeli kuliko wanawake wote;Mkewe Heberi, Mkeni,Atabarikiwa kuliko wanawake wote hemani.
25. Aliomba maji, naye akampa maziwa.Akamletea siagi katika sahani ya heshima.
26. Akanyosha mkono wake akashika kigingi,Nao mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi;Akampiga Sisera kwa hiyo nyundo, akamtoboa kichwa chake.Naam, alimpiga akamtoboa kipaji chake.
27. Miguuni pake aliinama, akaanguka, akalala.Miguuni pake aliinama, akaanguka.Hapo alipoinama, ndipo alipoanguka amekufa.
28. Alichungulia dirishani, akalia,Mama yake Sisera alilia dirishani;Mbona gari lake linakawia kufika?Mbona gurudumu za gari lake zinakawia?
29. Mabibi yake wenye akili wakamjibu,Naam, alijipa nafsi yake jawabu.
30. Je! Hawakupata mateka na kuyagawanya,Kijakazi, vijakazi wawili, kwa kila mtu?Kwa Sisera nyara ya mavazi ya rangi mbali mbali,Nyara za mavazi ya rangi mbali mbali ya darizi;Ya rangi mbali mbali ya darizi, pande zote mbili,Juu ya shingo za hao mateka.