2 Nya. 4:19-21 Swahili Union Version (SUV)

19. Basi Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu, madhabahu ya dhahabu pia, nazo meza, ambazo juu yake iliwekwa mikate ya wonyesho;

20. na vinara na taa zake, ziwake kama ilivyoagizwa mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu iliyosafika;

21. na maua, na taa, na makoleo, ya dhahabu, ndiyo dhahabu bora;

2 Nya. 4