2 Nya. 4:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Tena akafanya madhabahu ya shaba, mikono ishirini urefu wake, na mikono ishirini upana wake, na mikono kumi kwenda juu kwake.

2. Tena akaifanya bahari ya kusubu, mikono kumi toka ukingo hata ukingo, ya mviringo, na kwenda juu kwake ilikuwa mikono mitano; na uzi wa mikono thelathini kuizunguka kabisa.

3. Na chini yake palikuwa na mifano ya ng’ombe, walioizunguka pande zote, kwa mikono kumi, wakiizunguka pande zote ile bahari. Ng’ombe walikuwa safu mbili, wakayeyushwa hapo ilipoyeyushwa hiyo bahari.

4. Ikakaa juu ya ng’ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani.

5. Na unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu tatu, kukaa ndani yake.

2 Nya. 4