20. Mara Sauli akaanguka chini kifulifuli, akaingiwa na hofu kuu kwa sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yo yote; kwa maana hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha.
21. Ndipo yule mwanamke akamwendea Sauli, akamwona ya kuwa yeye ametaabika sana, akamwambia, Angalia, mjakazi wako ameisikiliza sauti yako, nami nimeutia uhai wangu mkononi mwangu, nami nimeyasikiliza maneno yako uliyoniambia.
22. Basi sasa, tafadhali, wewe uisikilize sauti ya mjakazi wako, nikakuandalie ngaa mkate kidogo; ukale, ili upate nguvu, utakapokwenda zako.
23. Lakini yeye alikataa, akasema, Mimi sitaki kula. Ila watumishi wake, pamoja na yule mwanamke, wakamlazimisha; naye akaisikiliza sauti yao. Basi akainuka hapo chini, akaketi juu ya kitanda.