1 Sam. 2:5-15 Swahili Union Version (SUV)

5. Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula,Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha.Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba,Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika.

6. BWANA huua, naye hufanya kuwa hai;Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.

7. BWANA hufukarisha mtu, naye hutajirisha;Hushusha chini, tena huinua juu.

8. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,Humpandisha mhitaji kutoka jaani,Ili awaketishe pamoja na wakuu,Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu;Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA,Naye ameuweka ulimwengu juu yake.

9. Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake;Bali waovu watanyamazishwa gizani,Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;

10. Washindanao na BWANA watapondwa kabisa;Toka mbinguni yeye atawapigia radi;BWANA ataihukumu miisho ya dunia;Naye atampa mfalme wake nguvu,Na kuitukuza pembe ya masihi wake.

11. Kisha Elkana akaenda Rama nyumbani kwake. Na yule mtoto akamtumikia BWANA mbele yake Eli, kuhani.

12. Basi, hao wana wa Eli walikuwa watu wasiofaa kitu; hawakumjali BWANA,

13. wala haki ya makuhani ilivyokuwa kwa watu. Wakati huo mtu ye yote alipotoa dhabihu wakati wo wote, ndipo huja mtumishi wa kuhani, nyama ilipokuwa katika kutokota, naye akawa na uma wa meno matatu mkononi mwake;

14. naye huutia kwa nguvu humo chunguni, au birikani, au sufuriani, au chomboni; nyama yote iliyoinuliwa kwa huo uma kuhani huichukua mwenyewe. Ndivyo walivyofanya huko Shilo kwa Waisraeli wote waliokuja huko.

15. Tena, kabla ya kuteketeza mafuta, huja mtumishi wa kuhani, akamwambia yule mwenye kuitoa dhabihu, Mtolee kuhani nyama ya kuoka; kwa kuwa hataki kupewa nyama iliyotokoswa, bali nyama mbichi.

1 Sam. 2