1 Nya. 24:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.

2. Lakini hao Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakafanya ukuhani.

3. Akawagawanya Daudi, na Sadoki wa wana wa Eleazari, na Ahimeleki wa wana wa Ithamari, katika utumishi kwa kadiri ya usimamizi wao.

4. Wakaonekana wakuu wengi wa wana wa Eleazari kuliko wa wana wa Ithamari; wakagawanyika hivi; wa wana wa Eleazari kulikuwa na kumi na sita, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao; na wa wana wa Ithamari, sawasawa na mbari za baba zao, wanane.

5. Ndivyo walivyogawanyika kwa kura, wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na wakuu wa Mungu, wa wana wa Eleazari, na wa wana wa Ithamari pia.

6. Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa mbari za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari mbari moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari.

7. Kura ya kwanza ikamtokea Yehoiaribu, na ya pili Yedaya;

8. ya tatu Harimu, ya nne Seorimu;

9. ya tano Malkia, ya sita Miyamini;

1 Nya. 24