25. Kwa kuwa Daudi alisema, BWANA, Mungu wa Israeli, amewastarehesha watu wake; naye hukaa Yerusalemu milele;
26. wala Walawi hawahitaji tena kuichukua maskani, na vyombo vyake vyote kwa utumishi wake.
27. Maana kwa maneno ya mwisho ya Daudi, hao wana wa Lawi walihesabiwa, wenye miaka ishirini na zaidi.
28. Kwani kazi yao ilikuwa kuwangojea wana wa Haruni katika utumishi wa nyumba ya BWANA, nyuani, na vyumbani, na kwa kuvisafisha vitakatifu vyote, ndiyo kazi ya utumishi wa nyumba ya Mungu;
29. tena kazi ya mikate ya wonyesho, na ya unga mwembamba wa sadaka ya unga; ikiwa ni wa maandazi yasiyochachwa, au wa yale yaliyotokoswa, au wa yale yaliyookwa; na kazi ya kila namna ya kipimo na cheo;
30. nao wasimame kila asubuhi kumshukuru na kumsifu BWANA, na jioni vivyo hivyo;
31. na kumtolea BWANA sadaka zote za kuteketezwa, katika siku za sabato, za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa, kwa hesabu kadiri ya agizo lake, daima mbele za BWANA;
32. tena walinde ulinzi wa hema ya kukutania, na ulinzi wa patakatifu, na ulinzi wa wana wa Haruni, ndugu zao, katika utumishi wa nyumba ya BWANA.