1 Nya. 15:21-27 Swahili Union Version (SUV)

21. na Matithiya, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, na Azazia, wenye vinubi vya sauti ya Sheminithi,

22. waongoze. Na Kenania, mkuu wa Walawi, alikuwa juu ya uchukuzi; yeye aliusimamia uchukuzi, kwa sababu alikuwa mstadi.

23. Na Berekia na Elkana walikuwa mabawabu kwa ajili ya sanduku.

24. Na Shebania, na Yoshafati, na Nethaneli, na Amasai, na Zekaria, na Benaya, na Eliezeri, makuhani, wakapiga baragumu mbele ya sanduku la Mungu; na Obed-edomu na Yehia walikuwa mabawabu kwa ajili ya sanduku.

25. Basi Daudi, na wazee wa Israeli, na maakida wa maelfu, wakaenda, ili kulipandisha sanduku la agano la BWANA kutoka nyumbani mwa Obed-edomu kwa furaha kuu;

26. hata ikawa, Mungu alipowajalia Walawi waliolichukua sanduku la agano la BWANA, wakachinja ng’ombe saba, na kondoo waume saba.

27. Naye Daudi alikuwa amevaa joho ya kitani safi, na Walawi wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.

1 Nya. 15