1 Kor. 13:3-12 Swahili Union Version (SUV)

3. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

4. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

5. haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

6. haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

7. huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

8. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

9. Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;

10. lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.

11. Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.

12. Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.

1 Kor. 13