1 Fal. 20:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi, Ben-hadadi mfalme wa Shamu akakusanya jeshi lake lote; nao walikuwapo wafalme thelathini na wawili pamoja naye, na farasi, na magari: akakwea akauhusuru Samaria, akaupiga vita.

2. Akatuma wajumbe kwa Ahabu mfalme wa Israeli, mjini, akamwambia, Ndivyo asemavyo Ben-hadadi.

3. Fedha yako na dhahabu yako ni zangu mimi; na wakezo na wanao, walio wema, ni wangu.

1 Fal. 20