4. Walakini kwa ajili ya Daudi, BWANA, Mungu wake, akampa taa humo Yerusalemu, amwinue mwanawe baada yake, na kuufanya imara Yerusalemu;
5. kwa sababu Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa BWANA, wala hakukosa katika yote aliyomwamuru, siku zote za maisha yake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti.
6. Basi kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote za maisha yake.
7. Na mambo yote ya Abiya yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
8. Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi. Akatawala Asa mwanawe mahali pake.
9. Mwaka wa ishirini wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa alianza kutawala juu ya Yuda.
10. Akatawala miaka arobaini na mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka, binti Absalomu.
11. Basi, Asa akafanya yaliyo mema machoni pa Mungu, kama alivyofanya babaye Daudi.