Yeremia 51:32-37 Biblia Habari Njema (BHN)

32. Vivuko vya mto vimetekwa,ngome zimechomwa moto,askari wamekumbwa na hofu.

33. Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema hivi:“Babuloni ni kama uwanja wa kupuria nafakawakati unapotayarishwa.Lakini bado kidogo tu,wakati wa mavuno utaufikia.”

34. Mfalme Nebukadneza wa Babulonialiuharibu na kuuponda mji wa Yerusalemualiuacha kama chungu kitupu;aliumeza kama joka.Alijaza tumbo lake vitu vyake vizurivizuri,akautupilia mbali kama matapishi.

35. Watu wa Yerusalemu na waseme:“Babuloni na ulipizwe ukatili uleule,tuliotendwa sisi pamoja na jamaa zetu!Babuloni ipatilizwekwa umwagaji wa damu yetu.”

36. Kwa hiyo asema hivi Mwenyezi-Mungu:“Nitawatetea kuhusu kisa chenu,na kulipiza kisasi kwa ajili yenu.Nitaikausha bahari ya Babulonina kuvifanya visima vyake vikauke.

37. Babuloni itakuwa rundo la magofu,itakuwa makao ya mbweha,itakuwa kinyaa na kitu cha kuzomewa;hakuna mtu atakayekaa huko.

Yeremia 51