Yeremia 30:17-20 Biblia Habari Njema (BHN)

17. “Nitakurudishia afya yako,na madonda yako nitayaponya,japo wamekuita ‘Aliyetupwa’,‘Mji Siyoni usio na wa kuutunza!’”

18. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nitazirudisha tena fanaka za maskani ya Yakobo,na kuyaonea huruma makao yake;mji utajengwa upya juu ya magofu yake,na ikulu ya mfalme itasimama pale ilipokuwa.

19. Humo zitatoka nyimbo za shukranina sauti za wale wanaosherehekea.Nitawaongeza na wala hawatakuwa wachache;nitawafanya waheshimiwe wala hawatadharauliwa.

20. Watoto wao watakuwa kama walivyokuwa zamani,jumuiya yao itaimarika mbele yangu,nami nitawaadhibu wote wanaowakandamiza.

Yeremia 30