15. Lakini watu wangu wamenisahau mimi,wanafukizia ubani miungu ya uongo.Wamejikwaa katika njia zao,katika barabara za zamani.Wanapitia vichochoroni badala ya njia kuu.
16. Wameifanya nchi yao kuwa kitisho,kitu cha kuzomewa daima.Kila mtu apitaye huko hushangaana kutikisa kichwa chake.
17. Nitawatawanya mbele ya adui,kama upepo utokao mashariki.Nitawapa kisogo badala ya kuwaonesha uso wangusiku hiyo ya kupata maafa yao.”
18. Kisha, watu wakasema: “Njoni tumfanyie Yeremia njama, maana hatukosi makuhani wa kutufundisha, wenye hekima wa kutushauri na manabii wa kututangazia ujumbe wa Mungu! Njoni tumshtaki kwa maneno yake mwenyewe, wala tusiyatilie maanani yote asemayo.”
19. Basi, mimi nikasali:Nitegee sikio ee Mwenyezi-Mungu,usikilize ombi langu.
20. Je, mtu hulipwa mabaya kwa mema?Walakini, wamenichimbia shimo.Kumbuka nilivyosimama mbele yako,nikasema mema kwa ajili yao,ili kuiepusha hasira yako mbali nao.