Sefania 3:13-19 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Waisraeli watakaobaki,hawatatenda mabaya wala hawatasema uongo;wala kwao hatapatikana mdanganyifu yeyote.Watapata malisho na kulalawala hakuna mtu atakayewatisha.”

14. Imba kwa sauti, ewe Siyoni,paza sauti ee Israeli.Furahi na kushangilia kwa moyo wote, ewe Yerusalemu!

15. Mwenyezi-Mungu amekuondolea hukumu iliyokukabili,amewageuzia mbali adui zako.Mwenyezi-Mungu, mfalme wa Israeli yuko pamoja nawehutaogopa tena maafa.

16. Siku hiyo, mji wa Yerusalemu utaambiwa:“Usiogope, ee Siyoni,usilegee mikono.

17. Mwenyezi-Mungu, Mungu wako yu pamoja naweyeye ni shujaa anayekuletea ushindi.Yeye atakufurahia kwa furaha kuu,kwa upendo wake atakujalia uhai mpya.Atakufurahia kwa wimbo wa sauti kubwa,

18. kama vile katika siku ya sikukuu.”Mwenyezi-Mungu asema:“Nitakuondolea maafa yako,nawe hutahitaji kuona aibu kwa ajili yake.

19. Wakati huo, nitawaadhibu wote wanaokukandamiza.Nitawaokoa vilema na kuwakusanya waliotupwa,na kubadili aibu yao kuwa sifana fahari duniani kote.

Sefania 3