Isaya 57:10-13 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Mlichoshwa na safari zenu ndefu,hata hivyo hamkukata tamaa;mlijipatia nguvu mpya,ndiyo maana hamkuzimia.

11. “Mlimwogopa na kutishwa na nanihata mkasema uongo,mkaacha kunikumbuka mimina kuacha kabisa kunifikiria?Mimi sikuwaambia kitu kwa muda mrefu;ndio maana labda mkaacha kuniheshimu!

12. Mnafikiri mnafanya sawa,lakini nitayafichua matendo yenu,nayo miungu yenu haitawafaa kitu.

13. Mtakapolia kuomba msaada,rundo la vinyago vyenu na liwaokoe!Upepo utavipeperushia mbali;naam, pumzi itavitupilia mbali.Lakini watakaokimbilia usalama kwangu,wataimiliki nchi,mlima wangu mtakatifu utakuwa mali yao.”

Isaya 57